ubuntuimpact
New

MADEREVA WA MALORI

TanzaniaTanzania·Dar es Salaammid
Other
0 views0 saves0 applied

Quick Summary

Overview

MAJUKUMU NA WAJIBU WA KAZI 1. Kusafirisha kwa usalama makontena na mizigo kati ya maeneo ya kampuni ya DCG, bandarini, na maeneo ya wateja kwa kuzingatia ratiba na njia zilizopangwa na kampuni. 2.

Technical Tools
Other
MAJUKUMU NA WAJIBU WA KAZI 1. Kusafirisha kwa usalama makontena na mizigo kati ya maeneo ya kampuni ya DCG, bandarini, na maeneo ya wateja kwa kuzingatia ratiba na njia zilizopangwa na kampuni. 2. Kufanya ukaguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kuhakikisha ubora wa gari, usafi, na uzingatiaji wa viwango vya usalama na matengenezo. 3. Kuhakikisha nyaraka za mizigo na usafirishaji zimekamilika, ni sahihi, na zinafuata taratibu husika. 4. Kupakia na kushusha mizigo kwa kushirikiana na timu za ghala na bandarini huku ukihakikisha mizigo inalindwa dhidi ya uharibifu au upotevu. 5. Kuhakikisha mizigo inafikishwa kwa wakati na kuwasiliana na kitengo cha usafirishaji au msimamizi endapo kutatokea ucheleweshaji, ajali, au mabadiliko ya njia. 6. Kufuatilia matumizi ya mafuta na kutoa taarifa za kilomita, matumizi ya mafuta, na dosari zozote kwa msimamizi. 7. Kuwasilisha uthibitisho wa uwasilishaji wa mzigo (POD) pamoja na nyaraka husika mara baada ya safari kukamilika. 8. Kuzingatia kikamilifu sheria za barabarani, sera za usalama za kampuni, na maadili ya udereva wakati wote. 9. Kuripoti hitilafu au matatizo ya kiufundi kwa kitengo cha matengenezo mara moja. 10.Kushiriki katika ratiba za matengenezo ya magari ili kuhakikisha huduma za kinga zinafanyika kwa wakati. 11.Kutunza kumbukumbu za safari, taarifa za uwasilishaji, na taarifa sahihi za muda wa kazi. 12.Kufanya majukumu mengine yatakayopangwa na msimamizi, ikiwemo kuendesha vifaa vingine kama Forklift, Wheel Loader, Excavator, na Bobcat inapohitajika. Requirements SIFA ZA MWOMBAJI 1. Awe na Leseni halali ya udereva ya Tanzania – Daraja E na C. 2. Awe na uzoefu wa miaka 3–5 katika kuendesha malori makubwa au magari ya kubeba makontena kwenye sekta ya usafirishaji au mizigo. 3. Awe na uelewa wa shughuli za bandarini na taratibu za forodha. 4. Mafunzo ya udereva wa kujihami (Defensive Driving) au usalama barabarani yatakuwa faida ya ziada. 5. Awe na nidhamu, uwajibikaji, na uwezo mzuri wa kutunza muda. 6. Awe na cheti cha udereva kutoka taasisi inayotambulika. 7. Elimu ya angalau kidato cha nne inapendekezwa. 8. Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA. 9. Awe tayari kufanya kazi za zamu za usiku. 10.Awe mwaminifu, mwenye kujisimamia, na mwenye kuwajibika binafsi. 11.Uwezo wa kuendesha vifaa kama Forklift, Wheel Loader, Excavator, na Bobcat utakuwa faida. 12.Ujuzi wa matengenezo ya magari makubwa au vifaa vizito utaongeza nafasi ya kuajiriwa. 13.Awe amehitimu mafunzo kutoka LATRA. Benefits MALIPO Kampuni itatoa mshahara na marupurupu ya ushindani kulingana na sheria za kazi. Mkataba wa kazi ni wa mwaka mmoja (1) na unaweza kuongezwa kulingana na utendaji wa kazi.

Location & Eligibility

Where is the job
Dar es Salaam, Tanzania
On-site at the office

Listing Details

Posted
June 22, 2026
First seen
June 22, 2026
Last seen
June 23, 2026

Posting Health

Days active
0
Repost count
0
Trust Level
52%
Scored at
June 22, 2026

Signal breakdown

freshnesssource trustcontent trustemployer trust

3 other jobs at ubuntuimpact

View all →

Explore open roles at ubuntuimpact.

Newsletter

Stay ahead of the market

Get the latest job openings, salary trends, and hiring insights delivered to your inbox every week.

A
B
C
D
Join 12,000+ marketers

No spam. Unsubscribe at any time.

ubuntuimpactMADEREVA WA MALORI